0

SABABU 7 ZINAZOKUFANYA USHINDWE KUWA NA PESA ZAKUTOSHA KATIKA MAISHA YAKO.
Katika maisha kuna wakati unaweza ukawa unajiuliza na pengine kushangaa kwanini umekuwa ni mtu ambaye huna pesa za kutosha wakati ukija kuchunguza maisha ya wanaokuzunguka ni watu wenye pesa na maisha yao wanayaendesha vizuri tu. Inawezekana ukawa unafanya kazi ama biashara nzuri inayokuingizia kipato cha kutosha lakini kutokana na sababu usizozijua huwa ukijikuta ni mtu wa kuishiwa na kujikuta kuwa huna pesa. Kama umekuwa ukiishi hivi na kuwa mtu wa kuishiwa na kushindwa kuwa na pesa za kutosha , makala hii ni muhimu sana kwako. Je, unajua ni sababu zipi zinakufanya ushindwe kuwa na pesa ya kutosha katika maisha yako?

HIZI NDIZO SABABU 7 ZINAZOKUFANYA USHINDWE KUWA NA PESA PESA ZAKUTOSHA KATIKA MAISHA YAKO.

1. Una tabia mbaya zinazokuzuia kupata pesa.
Kuwa na tabia mbaya zinazokuzuia kupata pesa, ni sababu mojawapo ambayo inasababisha wewe ushindwe kuwa na pesa za kutosha kukosha. Kama maisha yako yametawaliwa na tabia mbaya kama matumizi mabaya ya pesa, ulevi na kuangalia TV kwa muda mrefu, hali ambayo inakupelekea wewe kupoteza muda mwingi sana ambao ungekusaidia katika suala zima la uzalishaji, sahau kuwa na pesa. Hii inatokea ni kwa sababu tabia zako hizo zinakuwa hazikusaidii kukuzalishia zaidi ya kukufanya uzidi kuishiwa na kujikuta kukosa pesa katika maisha yako, mara kwa mara.

2. Unazungukwa na watu wengi ambao sio sahihi kwako.
Ili tuweze kufanikiwa na kuwa na mafanikio makubwa zaidi, tunahitaji kuwa na watu sahihi na waliofanikiwa zaidi yetu ili kuweza kutupa hamasa ya mafanikio. Katika maisha yako unapokuwa umezungukwa na watu wengi ambao ni hasi, hawaamini katika utajiri na mafanikio, ni lazima wewe utaanza kuwa kama wao kidogo kidogo na mwisho wa siku utajikuta umekuwa mtu ambaye na wewe unashindwa kuwa na pesa za kutosha kama wao. Kuzungukwa na watu wengi ambao sio sahihi kwako hii ni sababu mojawapo inayokusababisha wewe ushindwe kumudu kupata pesa.

3. Umekuwa mwongeaji sana bila kuchukua hatua.
Unapokuwa mwongeaji sana juu ya ndoto zako bila kuchukua hatua yoyote uwe na uhakika ni lazima mifuko yako iwe tupu, haina kitu. Watu wengi huwa ni waongeleaji wazuri sana wa ndoto na malengo waliyonayo, lakini linapokuja suala la vitendo inakuwa hakuna. Kama unatabia hii uwe na uhakika lazima pesa zitakupiga chenga, kwa sababu ndoto bila vitendo ni kazi bure. Wapo watu wengi sana hapa duniani ambao walikufa na kuzikwa na ndoto zao nzuri walizokuwa nazo bila kuzifanyia kazi. Jifunze kufanyia kazi ndoto zako, ili ubadili maisha yako.

4. Umekuwa hauna mipango maalumu.
Ni kitu ambacho unatakiwa ujiulize mara kwa mara katika maisha yako kuwa unataka kuwaje baada ya miaka michache kuanzia sasa? Unataka kuwa kama ulivyo sasa kwa kutegemea kazi ya aina moja? Ama una mipango gani mathubuti uliyojiwekea, ambayo itakusaidia uweze kuweza kuongeza kipato chako? Tatizo la watu wengi ambalo huwa lina sababisha moja kwa moja kuwa watu wa kushindwa kushindwa kupata pesa za kutosha katika maisha yao, linatokana na kuwa watu wakukosa mipango maalum itakayowaongoza kwenye uhuru wa kifedha.

5. Umekuwa ukikata tamaa mapema.
Kuwa na tabia ya kukata tamaa mapema kwa kile unachofanya, hiki ni kitu kingine ambacho kimekuwa kikikufanya uendelee kushindwa sana kupata pesa za kutosha katika maisha yako. Umekuwa ukikosa pesa kwa sababu, unakuwa unaachia fursa nyingi ambazo zingeweza kukusaidia kukupatia kipato cha kutosha. Kwa sababu ya kukata tamaa mapema unajikuta ukiwa ni mtu ambaye unapoteza pesa nyingi, ambazo zingeweza kukusaidia katika maisha yako.

6. Umekuwa ni mtu wa kupoteza muda sana.
Kama unaishi na unaendelea kuishi maisha ya kupoteza muda katika maisha yako huwezi kufanikiwa kwa chochote, zaidi utaendelea kuwa maskini. Watu wengi bila kujijua huwa ni watu wa kupoteza muda sana katika mambo yasiyo ya msingi kama mitandao ya kijamii, TV na mengineyo. Kwa kupoteza muda huko hushindwa kupangilia mambo ya msingi ambayo yangeweza kuwasaidia kuingiza kipato na matokea yake husababisha kuwa ni watu wa kushindwa kupata pesa. Kama unaishi maisha haya .. Kwa maelezo zaidi wasiliana nami; geffedavidyj@gmail.com
Brought to you with Geffe Davidy

Post a Comment

 
Top