0


By Sandra Brown TZA
onOctober 12, 2015 4SHARES COMMENTS

Msanii wa muziki wa Pop nchini Marekani, Janet Jackson anaziandika headlines kwenye stori za burudani siku ya leo… Nimetembelea mtandao wa Billboard na nimekutana na news kuhusiana na Janet Jackson ambayo ningependa kushare na wewe mtu wangu.

Je, unafahamu kuwa Janet Jackson ana jumla ya Album 7 toka aanze kufanya muziki miaka ya ’80? na je unajua ni album zake ngapi zimeshawahi kushika #1 moja kwenye chati ya Billboard 200 ya Marekani? kama hufahamu basi ichukue hii…

Janet Jackson ameibuka kwenye nafasi ya kwanza kwenye chati ya Billboard 200 na album yake mpya kabisa ‘Unbreakable’ ambayo ni album ya kwanza ya Janet baada ya kimya kingi kwa muda wa miaka 7, sio hayo tu… Billboard imemtaja Janet Jackson kama msanii wa tatu wa kike kuwa na Album 7 zilizoshika #1 ndani ya miaka 40!

Kwa mujibu wa mtandao wa Billboard na Nielsen Music, album mpya ya Janet Jackson ilitoka tarehe 2 October 2015  na ndani ya wiki ya kwanza tu album hiyo ilifanya mauzo ya juu sana!

Hii ni audio Album ya kwanza ya Janet Jackson toka Album yake  ya mwaka 2008 ‘Discpline’ambayo pia kwa mujibu wa Billboard, Album hiyo iliibuka kwenye nafasi ya #1 kwenye chati ya Billboard 200… Album nyingine za Janet Jackson zilizowahi kushika nafasi hiyo ni; All For You (2001), The Velvet Rope (1997), Janet. (1993), Janet Jackson’s Rhythm Nation 1814 (1989) na Control (1986).

Post a Comment

 
Top