Wazazi wa raia
mmoja wa Uingereza ambaye aliripotiwa kusafiri hadi nchini Iraq ili
kujiunga na Kundi la Islamic State wamebaini kwamba walikamatwa na
maafisa wa polisi.
Jack Lets mwenye umri wa miaka 20 kutoka
Oxford,ametajwa kuwa ''Jihadi Jack'' na magazeti kadhaa,ambayo
yameripoti kwamba aliondoka nchini Uingereza ili kujiunga na kundi hilo
wakati alipokuwa na miaka 18.John na Sally Letts walikiambia chombo cha habari cha Channel 4 kwamba walikamatwa baada ya kumtumia fedha za chakula na miwani mipya.
Msemaji amesema kuwa :Mwanamume mmoja wa miaka 55 na mwanamke wa miaka 53 kutoka Oxford walikamatwa kwa tuhuma za kutuma fedha nchini Syria ambazo zitatumika kwa maswala ya kigaidi,na waliotolewa hadi februari 17.
Post a Comment
Post a Comment