0

ZITTO: MAGUFULI hajawahi kukemea ufisadi  Akihojiwa na mtangazaji Tido Mhando katika kipindi cha mikikimikiki AZAM 2 TV leo asubuhi, Zitto ameshangazwa na hatua ya mgombea urais kupitia CCM kujipambanua kuuchukiaufisadi wakati kipindi chote cha mijadala ya ufisadi wa EPA, MEREMETA, BUZWAGI, TOKOMEZA, RICHMOND, ESCROW nk hakuwahi kukemea lolote. ZITTO alienda mbali zaidi kuhusiana na kauli ya Magufuli hivi karibuni akiwa Tanga kwamba atayarejesha mashamba ya mkonge kwa wananchi ilihali yeye Zitto alileta hoja hiyo ya mkonge bungeni na Magufuli aliungana na wenzie kuipinga hoja hiyo kwa macho makavu, leo anaudanganya umma kuwa atayarejesha ni usanii mkubwa.  Chanzo: AZAM II TV

Post a Comment

 
Top